Kingsley Coman
KLABU za Manchster United na Liverpool huenda zikamkosa winga wa Ufaransa, Kingsley Coman baada ya Bayern Munich kusema kwamba anaweza kuuzwa kwa bei ya pauni milioni 77. (Bild).

Jadon Sancho
HUKU makubaliano ya kumsaini winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho yakiafikiwa , kiungo wa West Ham, Declan Rice (22), beki wa Villareal mwenye umri wa miaka 24, Pau Torres na mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane (27) , ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer. (Guardian).

Leon Goretzka
MANCHESTER United pia ina azma ya kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Leon Goretzka (26), ambaye kandarasi yake na klabu hiyo ya Bundesliga inakamilika 2022. (Bild).

Espirito Santo
KLABU ya Tottenham imemuajiri aliyekuwa meneja wa Wolves, Nuno Espirito Santo kuwa bosi mpya kwa kandarasi ya miaka miwili.(Goal).

Raheem Sterling
MANCHESTER City ina mpango wa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa England, Raheem Sterling kuhusu hatma yake huku nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.
(Mail).

Nasser Al-Khelaifi
RAIS wa Paris St-Germain, Nasser Al-Khelaifi, amechukua nafasi ya mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo, Leonardo katika mazungumzo ya kumshawishi mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe kuongeza mkataba wake na klabu hiyo. Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 inakamilika 2022.(L’Equipe).

Erling Braut Haaland
MMILIKI wa Chelsea Roman Abramovich ana imani kwamba ‘The Blues’ inaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland (20), mwisho wa msimu huu. (Express).

Nuno Tavares
MCHEZAJI wa Ureno chini ya umri wa miaka 21, Nuno Tavares (21), atafanyiwa uchunguzi wa matibabu katika klabu ya Arsenal kabla ya kujiunga na washika bunduki kwa dau la pauni milioni saba akitokea Benfica. (Goal).

Lauren James
CHELSEA wamewasilisha ombi la mwisho kumsaini mshambuliaji wa Manchester United, Lauren James (19). (Goal).

Domenico Berardi
KLABU ya Leicester inakabiliwa na ushindani kutoka AC Milan katika kinyang’anyiro cha kumsaini winga wa Italia na Sassuolo, Domenico Berardi (26), ambaye amewavutia ‘The Azzurri katika michuano ya 2020. (Corriere dello Sport).

Dion Sanderson
NEWCASTLE United wamewasilisha ombi la pauni milioni 1.5 kumnunua beki wa Wolves, Dion Sanderson huku wakishindana na Sunderland kumsaini mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 21. (Mail).

Marcel Sabitzer
KLABU ya RB Leipzig itamuachia kiungo wa Austria, Marcel Sabitzer, kuondoka mwisho wa msimu huu kwa bei ya chini huku Arsenal, AC Milan na Roma zikimuwania kiungo huyo mchezeshaji mwenye umri wa miaka 27. (Bild).

James Tavernier
NAHODHA wa Rangers, James Tavernier, ananyatiwa na Manchester United, Brighton, Norwich na Arsenal. Mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 29 alitia saini kandarasi mpya mwezi Aprili , inayomfanya kusalia katika klabu hiyo hadi 2024. (90min).