Dani Ceballos
MUHISPANIA, Dani Ceballos (24), amesema, anataka kurejea La Liga msimu ujao baada ya mkataba wake wa mkopo Arsenal kutoka Real Madrid kumalizika. (Cadena SER).

Hector Bellerin
KLABU ya Juventus wanamtaka, Hector Bellerin na huenda wakamuachia tena kiungo wa Wales, Aaron Ramsey (30), katika mkataba wa kubadilishana wachezaji na washika bunduki.(Sport).

Nuno Espirito Santo
KOCHA wa zamani wa Wolves, Nuno Espirito Santo anakaribia kuteuliwa kuwa meneja wa Crystal Palace. (Telegraph).

Lorenzo Pellegrini
LIVERPOOL wametangaza dau la pauni milioni 25.8 kumnunua nahodha wa Roma na kiungo wa Italia, Lorenzo Pellegrini (24), kuchukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum (30). (Corriere dello Sport).

Saul Niguez
KLABU ya Atletico Madrid wamemtoa kiungo wa Hispania, Saul Niguez (26), kwa Manchester City ili wampate mshambuliaji wa Ureno, Bernardo Silva (26). (Times).

Erling Braut Haaland
MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund na Norway, Erling Braut Haaland (20), anapania kujiunga na Chelsea na yuko tayari kusubiri kwa mwaka mmoja kuhamia Stamford Bridge. (Telegraph).

Takumi Minamino
MSHAMBULIAJI wa Liverpool na Japan, Takumi Minamino, anahusishwa na kurejea Southampton ambako alikuwa kwa mkopo msimu uliopita baada ya kocha, Ralph Hasenhuttl, kuulizia mpango wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26. (HampshireLive).

Ruben Neves
KLABU ya Arsenal imefanya mazungumzo na Wolves kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa Ureno, Ruben Neves huku washika bunduki wakijiandaa kupanga orodha ya wachezaji wanaopigiwa upatu kujaza nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uswisi, Granit Xhaka (28), ambaye anakaribia kujiunga na Roma. (Goal).

Callum Hudson-Odoi
KLABU ya Bayern Munich imefufua mkakati wa kumsaka winga wa Chelsea na England, Callum Hudson-Odoi (20), mabingwa hao wa Ulaya wapo tayari kupokea ofa ya kumuuza. (Times).

Graham Potter
MENEJA wa Brighton, Graham Potter bado anagombea kuwa kocha mpya wa Everton baada ya Carlo Ancelotti kuondoka. (Athletic).

Brahim Diaz
AC Milan wamefahamishwa kwamba kumsaini kiungo wa Hispania, Brahim Diaz (21), kwa mkataba wa kudumu kutoka Real Madrid kutawagharimu euro milioni 26, lakini, klabu hiyo ya ‘La Liga’ ipo tayari kumtoa tena kwa mkopo nyota huyo. (Goal).

Ben White
KLABU ya Brighton anatarajia kuzuia nia ya beki wa England, Ben White kutoka kwa klabu kama Manchester United, Arsenal na Liverpool kwa kuweka uthamini wa pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Mail).

Odsonne Edouard
LEICESTER City wamekubali uhamisho wa pauni milioni 15 na Celtic kwa mshambuliaji wa Ufaransa, Odsonne Edouard (23). (Sun).