Kingsley Coman
MTENDAJI wa Bayern Munich, Oliver Kahn, ana uhakika wa kumbakisha klabuni hapo winga Mfaransa, Kingsley Coman, licha ya Liverpool kuonyesha nia ya kumtaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 25. (Mirror).

Sergio Ramos
MLINZI wa Hispania, Sergio Ramos (35), atafanyiwa vipimo vya afya jijini Paris kabla ya kujiunga na Paris St-Germain kama mchezaji huru kufuatia kuondoka kwake Real Madrid. (ESPN).

Eduardo Camavinga
MANCHESTER United wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 50 kwa ajili ya mlinzi wa Real Madrid, Mfaransa Raphael Varane (28), na pauni milioni 25 kwa ajili ya kiungo wa Ufaransa anayekipigia Rennes, Eduardo Camavinga (18), huku wakiendelea kumwaga fdha kujenga kikosi chao. (Marca).

Mario Balotelli
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester City, Mario Balotelli (30), anajiandaa kujiunga na klabu ya Adana Demirspor ya Uturuki, akiwa na imani ya kurejea kwenye timu ya taifa kwa ajili ya fainali za mwakani za Kombe la Dunia. (Goal).

Lionel Messi
KLABU ya Paris St-Germain imempa ofa ya kumpeleka Ufaransa, Muargentina Lionel Messi baada ya mkataba wake na Barcelona kukoma wiki iliyopita. Gwiji huyo wa Nou Camp mwenye umri wa miaka 33 ameisaidia nchi yake kufuzu nusu fainali ya Copa America licha ya sintofahamu ya mustakabali wake. (Mail).

Antoine Griezmann
MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Mfaransa Antoine Griezmann (30), anaonekana kuwa chaguo linalowezekana kwa Manchester City msimu huu iwapo miamba hiyo itashindwa kumnasa mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs na England, Harry Kane (27). (Mundo Deportivo).

Paul Pogba
JUVENTUS wanataka kumrejesha kiungo wake za zamani anayechezea Manchester United, Paul Pogba (28), msimu huu. Wakali hao wa Italia wanataka kumrejesha Turin mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa miaka mitano tangu aondoke kwa uhamisho ulioweka rekodi ya dunia. (90Min).

Tiemoue Bakayoko
AC Milan wanajiandaa kuanza mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho mwengine wa mkopo wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Tiemoue Bakayoko (26). (Corriere dello Sport).

Kylian Mbappe
LIVERPOOL inaongoza harakati za majaribio ya kutaka kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa na PSG, Kylian Mbappe. Tetesi zinaendelea kuhusu mustakabali wa kinda hilo lenye umri wa miaka 22 ambaye amebakisha mwaka mmoja tu wa mkataba wake pale Parc des Princes. (ESPN).

Patrick Vieira
MENEJA mpya wa Crystal Palace, Patrick Vieira ana matumaini kwamba kiungo wa Scotland na Celtic, Ryan Christie atakuwa usajili wake wa kwanza Selhurst Park. Nyota huyo mwenye miaka 26 anawaniwa pia na klabu ya zamani ya Vieira, Nice. (Daily Record).

Emile Smith Rowe
KOCHA wa Arsenal Mikel Arteta ana uhakika wa kumbakisha, Emile Smith Rowe hapo Emirates, licha ya ushawishi mkubwa kutoka Aston Villa. Villa inajiandaa kuongeza dau kwa ajili ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 20, baada ya dau la mwanzo la pauni milioni 30 kukataliwa. (Mirror).

Haris Seferovic
KOCHA mpya wa Tottenham Hotspurs,Nuno Espirito Santo, anataka kumnasa mshambuliaji wa Switzerland,Haris Seferovic. Benfica inataka kumpiga bei mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Mirror).

Kostas Tsimikas
KLABU ya Inter Milan ina matumaini ya kumsajili mlinzi wa kushoto wa Kigiriki, Kostas Tsimikas kutoka Liverpool. Tsimikas (25), alijiunga na Liverpool msimu uliopita, na mpaka sasa amefanikiwa kuichezea klabu hiyo michezo saba tu katika mashindano yote. (Calciomercato).