Samuel Umtiti
MANCHESTER United na Arsenal wanataka kumsajili mlinzi wa kati wa Barcelona, Samuel Umtiti. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 27 anaonekana kutokwenda sawa na mipango ya meneja Ronald Koeman. (Star).

Raheem Sterling
NYOTA wa Manchester City na England, Raheem Sterling yuko tayari kusikiliza ofa ya kuondoka klabuni hapo. Lakini meneja Pep Guardiola anataka winga huyo mwenye umri wa miaka 26 kubakia Etihad, licha ya Real Madrid kuonyesha kumuhitaji. (Athletic).

Gareth Bale
WINGA, Gareth Bale (31), anaweza kustaafu kucheza soka la klabu mara baada ya mkataba wake mnono na Real Madrid anaolipwa pauni 600,000 kwa wiki utakapokoma msimu ujao. Kumekuwa na tetesi nyingi tangu kurejea kwa mshambuliaji huyo wa Wales aliyekuwa anacheza kwa mkopo Tottenham. (Mail).

Morgan Rogers
KLABU ya Crystal Palace imeanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, Muingereza Morgan Rogers (18). Kocha mpya wa klabu hiyo, Patrick Vieira anataka kuimarisha na kuweka sawa uwiano wa umri katika kiosi hicho msimu huu. (Mail).

Kalvin Phillips
KIUNGO wa Leeds na England, Kalvin Phillips (25), ana furaha kwenye klabu yake na hana mpango wa kuikacha kwa mujibu wa wakala wake. (The Newspaper).

Edmond Tapsoba
KLABU za Chelsea na Arsenal zinamfuatilia mlinzi wa Bayer Leverkusen na Burkina Faso, Edmond Tapsoba. Lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amewaambia waandishi wa habari kwamba ‘hakuna ofa ya uhakika na rasmi’ iliyowasilishwa kwake, kwa maana hiyo ataendelea kuwa na wajerumani hao msimu mpya utakapoanza. (Metro).

Emile Smith Rowe
KLABU ya Aston Villa inaamini kwamba inaweza kumpata kiungo wa Arsenal, Emile Smith Rowe na watawasilisha dau jengine la tatu kwa ajili ya Muingereza huyo. (Football Insider).

Ben White
KLABU ya Arsenal inaendelea kumshawishi mlinzi wa Brighton, Ben White (23), ambapo tayari imeshawasilisha dau la pauni milioni 50 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England. Hata hivyo inaelezwa kwamba dau hilo halijakubalika kama inavyoripotiwa na vyombo vingi vya habari. (Argus).

Brandon Williams
KLABU ya Southampton ina uhakika wa kukamilisha uhamisho wa mkopo wa mlinzi wa Manchester United, Brandon Williams. Saints walimtaka kinda hilo la Kiingereza lenye umri wa miaka 20 tangu msimu uliopita, lakini, United hawakutaka kumruhusu kuondoka. (Mail).

Wayne Hennessey
KLABU ya Burnley imeonyesha nia ya kumtaka Wayne Hennessey, aliye huru. Mlinda mlango huyo wa Wales mwenye umri wa miaka 34 anatakiwa pia na klabu za Chelsea na Aston Villa baada ya kuondoka Crystal Palace mwezi uliopita kufuatia kumalizika kwa mkataba wake. (Mail).

Antoine Griezmann
BARCELONA itawapa nafasi Chelsea ya kumsajili mshambuliaji wake, Antoine Griezmann. Magwiji hao wa Catalunya wanaokabiliwa na tatizo la kifedha wanataka kumpiga bei Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 30 ili kukamilisha mkataba mpya wa Lionel Messi. (Star).

Joan Laporta
HAHA hivya Rais wa Barcelona, Joan Laporta, amesema, kila kitu kinakwenda sawa, licha ya mkataba huo wa Messi (34), kumalizika na kumfanya kwa mchezaji huru. (Marca).