Franck Kessie
AC Milan itaongeza dau lake kwa ajili ya kiungo wa Ivory Coast, Franck Kessie wakijaribu kuongeza mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24. (Gazzetta dello Sport).

Erling Braut Haaland
CHELSEA wanajiandaa kutoa kitita cha pauni milioni 150 kwa ajili ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland na tayari klabu hiyo ya Stamford imeshafanya mazungumzo na upande wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway. (90 Min).

Pep Guardiola
MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema, klabu hiyo haiwezi kumudu gharama za mshambuliaji mpya na kuna kila dalili mabingwa hao wa Ligi Kuu England wasisajili mshambuliaji msimu huu. (TVS).

Richarlison
MENEJA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, amesema, angelitamani kumsajili mshambuliaji wa Kibrazil, Richarlison (24), kutoka klabu yake ya zamani ya Everton. Klabu hiyo ya ‘La Liga’ inaangalia kama hilo linawezekana. (ESPN).

Jorginho
WAKALA wa kiungo wa Chelsea, Jorginho (29), amesema zipo timu zinazomuhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia, lakini, anatarajiwa kuongeza mkataba mpya wa kusalia ‘The Blues’ zaidi ya mwaka 2023. (Radio Marte).

Marcel Sabitzer
NAHODHA wa RB Leipzig, Marcel Sabitzer (27), anaweza kupatikana kwa ada ya pauni milioni 17 wakati huu kiungo huyo wa Austria akiingia miezi yake 12 ya mwisho ya mkataba wake na mazungumzo kuhusu mkataba mpya yakiwa bado yanasuasua. (90 Min).

Ruben Vinagre
KLABU ya Wolves imekubali kumuuza beki wake wa Kireno, Ruben Vinagre (22), kwenda Sporting Lisbon kwa ada ya pauni milioni 8.6. (Football Insider).

Mert Muldur
TOTTENHAM Hotspurs wanamfuatilia beki wa Sassuolo, Mert Muldur, huku West Ham wakitajwa kumtaka pia nyota huyo wa kimataifa wa Uturuki mwenye umri wa miaka 22. (Mail).

Sergio Ramos
KLABU ya Paris St-Germain imejikuta kwa bahati mbaya ikithibitisha kumsajili beki wa kati wa Hispania, Sergio Ramos (35) ambaye ameondoka Real Madrid baada ya mkataba wake kumalizika, kwa kuchapisha usajili wake kwenye mtandao wa klabu hiyo kabla ya muda uliopangwa. (Goal).

Adam Armstrong
KLABU ya Southampton ina uhakika wa kunasa saini ya mshambuliaji wa Kiingereza, Adam Armstrong (24), kutoka Blackburn Rovers kwa ada ya pauni milioni 10. (Football League World).

Martin Payero
KLABU ya Middlesbrough ipo katika mazungumzo mazuri ya kumsajili kiungo wa Atletico Banfield, Martin Payero ambaye yumo kwenye kikosi cha Argentina kitakachoshiri michezo ya Olimpiki huko Tokyo msimu huu. (Football Insider).

Leon Goretzka
MENEJA wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann, amesema kiungo wa Ujerumani, Leon Goretzka, anayehusishwa kutakiwa Manchester United, ni mchezaji muhimu wa klabu hiyo na atafurahi kufanya naye kazi kwa miaka mingi ijayo. (Goal).

Davide Calabria
KIUNGO wa Italia, Davide Calabria (24), amekubali kusaini mkataba mpya utakaombakisha AC Milan mpaka 2025. (Calciomercato).