HARRY KANE
MANCHESTER UNITED wanaongoza Chelsea na majirani zao Manchester City katika kinyang’anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa England Harry Kane, 27. Tottenham inataka pauni milioni 100 na wachezaji wawili wa wa kikosi cha kwanza cha Red Devils. (Football Insider)
ANTOINE GRIEZMANN
MANCHESTER CITY wamewasiliana na mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 30, kuhusu uwezekano wa uhamisho kutoka Barcelona. (Footmercato – in French)
ALPHONSE AREOLA,
WEST HAM wanashauriana na Paris St-Germain kuhusu usajili wa kipa wa Ufaransa aliye na umri wa miaka 28- Alphonse Areola, ambaye alikuwa Fulham kwa mkopo msimu uliopita. (Mail)
MARKO ARNAUTOVIC
UHAMISHO wa mshambuliaji wa Austria Marko Arnautovic kwenda Bologna kutoka Shanghai SIPG umekwama, kufuatia utata unaozunguka kanuni ya mkataba wa mchezaji huyo wa zamani wa West Ham na Stoke City kuhama klabu hiyo ya China. (Bild – kwa Kijerumani)
EMILE SMITH ROWE
KIUNGO wa kati wa Arsenal na England kwa wachezaji waliyo na chini ya miaka -21 Emile Smith Rowe, 20,anajiandaa kusaini mkataba wa miaka mitano Gunners. (Birmingham Mail)
KURT ZOUMA
KURT ZOUMA anatarajiwa kuondoka Chelsea msimu huu wa joto, huku Everton, Tottenham na Roma zikimtaka Mfaransa huyo aliye na umri wa miaka 26, ambaye tayari amekataa ombi kutoka Wolves.(Telefoot on Twitter)
MATTHEW HOPPE
NEWCASTLE UNITED, Tottenham, Wolves na Southampton wnajiandaa kuwasilisha la kumnunua mshambuliaji wa Schalke na Marekani Matthew Hoppe,20. (90min)
MIKKEL
SAMPDORIA wanaimani ya kusalia na mshambuliaji wa Denmark Mikkel, 21, walau kwa msimu mwingine, huku Liverpool, Tottenham, Juventus na Barcelona zikiwa miongoni mwaka klabu zinazomnyatia nyota huyo . (Gazzetta dello Sport – in Italian)
SON HEUNG-MIN
MKURUGENZI wa kandanda wa Tottenham Fabio Paratici ameamua mkataba mpya wa kudumu wa mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min, 29, kuwa kipaumbele chake. (90min)
SAMUEL UMTITI
MANCHESTER UNITED ”wanataka” kumsajili mlinzi wa Barcelona Samuel Umtiti ,27, huku Arsenal pia wamehusishwa na usajili wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa l. (El Gol – in Spanish)
KIKO CASILLA
Kipa wa Hispania Kiko Casilla, 34, anataka kuondoka Leeds United kujiunga na klabu ya La Liga ya Elche kwa sasabu ya kukosa nafasi ya kucheza Elland Road. (Mirror).
CRISTIAN ROMERO
BARCELONA na Tottenham wameungana na Manchester United katika mbio za kumsaka mlinzi wa Argentina Cristian Romero, ambaye yuko kwa mkopo Atalanta kutok Juventus. (Calciomercato – in Italian)