ZASPOTI
Andre Onana
ARSENAL inaendelea kumuangalia mlinda mlango wa Ajax, Andre Onana, lakini, wanahofu nyanda huyo anapendelea kuhamia Lyon.
Washika bunduki wanataka kuleta kipa mpya msimu huu wa joto na wamefanya, Onana kuwa mlengo wao wa kwanza.(Football.London).
Carles Alena
BARCELONA wamekubali mpango wa kumuuza, Carles Alena kwenda Getafe huku wakiendelea na zoezi lao la kupunguza gharama ili kuhakikisha wanaweza kumsajili, Lionel Messi juu ya mkataba mpya.
Kanuni za mishahara ya ‘La Liga’ zinamaanisha kwamba Barca kwa sasa hawawezi kusajili usajili wowote mpya au kukubali mkataba mpya na Messi ambaye mkataba wake wa awali ulimalizika mwishoni mwa mwezi uliopita.(Marca).
Ryan Christie
KLABU ya Sampdoria inaangalia uhamisho wa kushangaza kwa kiungo wa Celtic, Ryan Christie.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland amemaliza mkataba mnamo Januari hivyo anaweza kusaini makubaliano ya mkataba wa mapema sasa. (Daily Record).
Kurt Zouma
BEKI wa Chelsea, Kurt Zouma, anatarajiwa kuondoka Stamford Bridge msimu huu wa joto.
Mfaransa huyo tayari amekataa azma kutoka Wolves, lakini, Everton, Tottenham na Roma zote zinaendelea kuvutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Telefoot).
Jules Kounde
KLABU ya Tottenham imepania kupambana na Real Madrid katika mbio za kumsajili beki wa Sevilla, Jules Kounde.
‘Los Blancos’ wana azma ya kuimarisha ulinzi wao kufuatia kuondoka kwa Sergio Ramos na kutarajiwa kuondoka kwa Raphael Varane.(Sports).
Alphonse Areola
WEST Ham wanashauriana na Paris St-Germain kuhusu usajili wa kipa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28, Alphonse Areola ambaye alikuwa akikipiga Fulham kwa mkopo msimu uliopita. (Mail).
Marko Arnautovic
UHAMISHO wa mshambuliaji wa Austria, Marko Arnautovic kwenda Bologna kutoka Shanghai SIPG umekwama, kufuatia utata unaozunguka kanuni ya mkataba wa mchezaji huyo wa zamani wa West Ham na Stoke City kuhama klabu hiyo ya China. (Bild).
Emile Smith Rowe
KIUNGO wa Arsenal na England chini ya miaka 21, Emile Smith Rowe (20), anajiandaa kusaini mkataba wa miaka mitano na washika bunduki. (Birmingham Mail).
Matthew Hoppe
KLABU za Newcastle United, Tottenham, Wolves na Southampton zinajiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Schalke na Marekani, Matthew Hoppe (20). (90min).
Cristian Romero
KLABU ya Barcelona na Tottenham wameungana na Manchester United katika mbio za kumsaka mlinzi wa Argentina, Cristian Romero, ambaye yuko kwa mkopo Atalanta kutoka Juventus. (Calciomercato).