KALIDOU KOULIBALY
KOCHA wa Everton Rafa Benitez amewahimiza wakuu wa klabu kumsajili mlinzi wa kati wa Napoli, Msenegali Kalidou Koulibaly, 30. (90min)
FABIAN RUIZ
NAPOLI wanataka kuwaachilia Koulibaly, kiungo wa kati wa Hispania Fabian Ruiz, wakati wakijaribu kupunguza fedha zinazotumiwa kuwalipa mishahara wachezaji , hata hivyo hawajapokea ofa yoyote kwa wachezaji hao. (Calciomercato – in Italian)
LIONEL MESSI
MSHAMBULIAJI wa Argentina Lionel Messi yuko mbioni kusalia na Barcelona, huku mchezaji huyo mwenye miaka 34 akitarajiwa kusaini mkataba na klabu hiyo ya Catalonia. (AS)
GABRIEL JESUS
MSHAMBULIAJI wa Manchester City Gabriel Jesus, 24, amekuwa pendekezo la kwanza la Juventus wakiwa na nia ya kuimarisha safu ya ushambuliaji msimu ujao, lakini kumrejesha Moise Kean Turin kutoka Everton ni suala la hiari. (Tuttosport – in Italian)
ANDRE ONANA
MATUMAINI ya Arsenal kumsajili mlinda mlango wa Ajax Andre Onana yamepata pigo baada ya mchezaji huyo kukubali masharti binafsi na Lyon. Klabu hizo mbili hata hivyo hazijafikia makubaliano. (Fabrizio Romano – via Sun)
RUBEN NEVES
ARSENAL wameanza mazungumzo na Wolves kwa ajili ya kumpata kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 24. (Record – in Portuguese)
GIORGIO CHIELLINI
MLINZI wa Italia mwenye umri wa miaka 36 Giorgio Chiellini atasaini nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja na Juventus wiki ijayo, na kusalia na klabu ya Turin hadi Juni 2022. (Fabrizio Romano kwenye Twitter)
PATRICK VIEIRA
KOCHA wa Crystal Palace, Patrick Vieira anageukia klabu yake ya zamani kupata wachezaji wapya, huku Arsenal ikivutiwa sana na mshambuliaji wa Gunners wa chini ya miaka 21 Eddie Nketiah, 22, na mshambuliaji wa Denmark Kasper Dolberg, 23, kutoka Nice timu iliyokuwa ikifundishwa na Mfaransa huyo. (Sun)
ARNAUT DANJUMA
BOURNEMOUTH imekataa dau la pauni milioni 13 kutoka Villarreal kwa ajili ya winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma.(Sky Sports)
HARRY WILSON
WAGENI wapya wa Ligi ya England Brentford wanajiandaa kutengeneza kitita cha pauni milioni 10 kumnasa mshambuliaji wa Liverpool na Wales mwenye umri wa miaka 24 Harry Wilson. (Sun)
ISMAIL JAKOBS
MSHAMBULIAJI wa chini ya miaka 21 wa Cologne ya Ujerumani Ismail Jakobs, 21, anatarajiwa kujiunga na Monaco, hapo awali alihusishwa na taarifa za uwezekano wa kuhamia Leicester City na Brighton. (Sky Sport Germany)
ANDREA BELOTTI
MSHAMBULIAJI wa Italia Andrea Belotti ataamua ikiwa atasaini tena mkataba wake na Torino mara tu baada ya fainali ya Mashindano ya Uropa. Kocha wa Roma ya Jose Mourinho ana shauku ya kumsajili mchezaji huyo wa miaka 27 ikiwa ataondoka. (Sky Sport Italia – kwa Kiitaliano)
FAMARA DIEDHIOU
SWANSEA CITY na Middlesbrough wamehusishwa na uhamisho wa mshambuliaji wa Senegal Famara Diedhiou, 28, ambaye aliondoka Bristol City mwishoni mwa mkataba wake mapema msimu wa joto. (Football Insider)