Lorenzo Pellegrini
KLABU ya Tottenham inaweza kumsajili kiungo wa kati wa Roma, Lorenzo Pellegrini (25), lakini, watatakiwa kutoa kititia cha pauni milioni 26 kumnasa Muitaliano huyo. (Athletic ).

Tammy Abraham
ARSELA wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea, Tammy Abraham (23) ambaye ‘The Blues’ pia wameashiria kuwa tayari kumuuza Tottenham na Inter Milan. Chelsea wanawalenga mshambuliaji wa Spurs na England Harry Kane mwenye umri wa miaka 27 na Romelu Lukaku wa Inter na Ubelgiji. (Telegraph).

Mohamed Salah
KOCHA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti anawataka viongozi wa klabu hiyo kumsajili mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah (29), anayekipiga Liverpool ikiwa mchakato wa kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain, Kylian Mbappe utakwama msimu huu wa joto. (Fichajes).

Danny Ings
KLABU ya Tottenham wanamtaka mshambuliaji, Danny Ings, lakini, wanakabiliwa na ugumu kwa sababu Southampton wanasita kufanya biashara na klabu hiyo ya kaskazini mwa London. (Standard).

Jesse Lingard
MABINGWA wa Hispania, Atletico Madrid wamekuwa wakihusishwa na taarifa za kutaka kumsajili kiungo wa Manchester United, Jesse Lingard, ambaye pia anatolewa macho na West Ham ambao walipendezwa naye alipokuwa kwa mkopo msimu uliopita. (90min).

Dusan Vlahovic
KLABU ya Fiorentina inalenga kuzuia kupokonywa nyota wao, Dusan Vlahovic ambaye anamezewa mate na Liverpool na Tottenham kwa kuhakikisha wanampa mshambuliaji huyo wa Serbia mkataba mpya.(Calciomercato).

Raphael Varane
REAL Madrid wameridhia kuwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Raphael Varane hatasaini mkataba mpya na wanasubiri ofa ya Manchester United. (Goal).

Kristoffer Ajer
KLABU ya Brentford inajiandaa kuweka mezani ofa ya ya pauni milioni 13.5 kwa ajili ya mlinzi wa Celtic, Kristoffer Ajer (23). (Sun).

Mathias Olivera
MLINZI wa Chelsea, Emerson Palmieri (26), anatakiwa na Inter Milan na Roma, huku akiwa chaguo pendwa kwa Napoli wakati pia wakimtolea macho, Mathias Olivera (23), anayekipiga Getafe. (Calciomercato).

Joe Willock
KUMSAJILI mchezaji wa Arsenal, Joe Willock (21), kwa mkataba wa kudumu bado imekuwa kipaumbele cha Newcastle United msimu huu baada ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21, kuwepo St James Park kwa mkopo msimu uliopita. (Chronicle).

Theo Hernandez
AC Milan wamekataa ofa ya pauni milioni 34 kutoka Paris St-Germain kwa ajili ya kiungo wa Ufaransa, Theo Hernandez mwenye umri wa miaka 23. (Tuttosport).

Nicolo Barella
KLABU ya Inter Milan imeisitiza kuwa kiungo, Nicolo Barella, hataguswa baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 atahamia Liverpool na
Manchester United. (Fabrizio Romano on Twitter).

Kalidou Koulibaly
EVERTON imewasilisha dau la mwanzo kumsajili mchezaji wa Napoli na Senegal, Kalidou Koulibaly (30) ambaye anaripotiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na maneja Rafa Benitez. (Calciomercato).