Nicolo Fagioli
KIUNGO wa Juventus, Mtaliano Nicolo Fagioli (20), ambaye ni sehemu ya mkataba wa kubadilishana mchezaji wa Sassuolo, Manuel Locatelli, amethibitisha mahasimu wao Arsenal wamewasilisha dau la pauni milioni 34 kumnunua. (Sky Italy).

Paul Pogba
KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba ananyatiwa na Paris St-Germain msimu huu wa joto na klabu hiyo ya ‘Ligue 1’ inapanga kuwauza wachezaji kadhaa kukusanya pauni milioni 50 wanazoamini zitafanikisha azma ya kumpata nyota huyo. (Mirror).

Lionel Messi
BARCELONA wanajikakamua kuuza wachezaji ili kufadhili mkataba wa mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi (34), kabla ya msimu mpya kuanza. (Guardian).

Rapahel Varane
BEKI wa Real Madrid na Ufaransa, Raphael Varane (28), ana matumaini uhamisho wake kwenda Manchester United utakamilishwa siku chache zijazo. (AS).

Reiss Nelson
ARSENAL wapo tayari kuipatia Leicester City wachezaji kadhaa akiwemo winga, Muingereza Reiss Nelson (21) kama sehemu ya mkataba wa kumsaini kiungo wa England, James Maddison (24). (Daily Mail).

Neto
KLABU ya Arsenal wameimarisha juhudi za kumsaka kipa wa Barcelona, Mbrazil Neto (31). (Mundo Deportivo).

Erling Braut Haaland
CHELSEA huenda wakawasilisha dau la pauni 135 kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway, Erling Braut Haaland (20). (ESPN).

Bryan Gil
KLABU ya Tottenham inakaribia kufikia makubaliano na winga wa Sevilla, Mhispania Bryan Gil ambao utamwezesha mshambuliaji wa Argentina, Erik Lamela kuhamia klabu hiyo ya La Liga. (Sky Sports).

Kieran Trippier
MANCHESTER United wana nafasi ya kuwasajili wachezaji wakubwa wawili kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa wiki sita zijazo. Beki wa Atletico Madrid na England, Kieran Trippier ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa. (Manchester Evening News).

Cristian Ronaldo
JUVENTUS wanatathmini uwezekano wa mkataba wa kubadilishana wachezaji ambao utamwezesha Cristiano Ronaldo (36), kujiunga na PSG nao wampate tena mshambuliaji wa Argentina, Mauro Icardi (28). (L’Equipe via Daily Star).

Merih Demiral
KLABU ya Juventus wameweka pauni milioni 35 kuwa bei ya kumuulizia mlinzi wa Uturuki Merih Demiral, ambaye anahusishwa na uhamisho wa kwenda Everton. (Goal).

Lewis Bate
LEEDS United wanapigiwa upatu kumsajili kiungo wa Chelsea, Muingereza Lewis Bate (18). (Daily Mail).

Demarai Gray
WINGA wa Bayer Leverkusen, Demarai Gray (25), alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu juzi anapokaribia kusajiliwa na Everton. (Sky Sports).

Marcus Bettinalli
KLABU ya Chelsea wanamtaka kipa wa zamani wa Fulham, Marcus Bettinelli (29), kujiunga nao msimu ujao. (The Telegraph).