Robert Lewandowski
CHELSEA imezUngumza na ajenti wa mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland, Robert Lewandowski (32), kuhusu uwezekano wa kumleta Stamford Bridge. (Bild).
Aaron Ramsdale
ARSENAL inajiandaa kuwasilisha dau la pauni milioni 30 kumnunua kipa wa Sheffield United, Muingereza Aaron Ramsdale (23). (TalkSport).
Tammy Abraham
CHELSEA ipo tayari kumuachia mshambuliaji, Tammy Abraham kujiunga na mahasimu wao wa Ligi Kuu ya England, Arsenal kwa mkopo. Tottenham na West Ham pia wanamnyatia kiungo huyo mahiri mwenye umri wa miaka 23. (Sun).
Timo Werner
MSHAMBULIAJI wa Ujerumani, Timo Werner (25), ameanzisha mazungumzo ya kuondoka Chelsea msimu huu wa joto. Kuna uwezekano akarejea katika ligi ya nyumbani ya Bundesliga. (90min).
Nat Phillips
LIVERPOOL huenda wakamuuza kiungo, Nat Phillips (24), winga wa Wales, Harry Wilson (24), mshambuliaji wa Ubelgiji, Divock Origi (26), beki wa Wales, Neco Williams (20), na kiungo wa Uswizi, Xherdan Shaqiri (29), katika mpango wa kukusanya kati ya pauni milioni 60 hadi 70. (Liverpool Echo).
Paul Pogba
PARIS St-Germain wanamtaka kiungo wa Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba (28), lakini klabu hiyo ya Ufaransa itahitajika kuwauza baadhi ya wachezaji wake kwanza. (Sky Sports).
Ruben Neves
KLABU ya Manchester United ipo mbele ya Arsenal kwenye mchakato wa kumsajili kiungo wa Ureno, Ruben Neves (24), kwa kiasi cha pauni milioni 35 kutoka Wolves msimu huu wa joto. (TalkSport).
Leon Goretzka
MANCHESTER United wamempatia kiungo wa Ujerumani, Leon Goretzka ofa ya pauni 200, 000 kwa wiki ili kumsaini wakati mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 26utakapokamilika Bayern Munich msimu ujao.(Daily Mail).
Todd Cantwell
KLABU ya Aston Villa wamepiga hatua katika mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Norwich City mwenye umri wa miaka 23, Todd Cantwell. (Football Insider).
Leon Bailey
ASTON Villa pia wapo tayari kumnunua winga wa Bayer Leverkusen, Mjamaica Leon Bailey (23), ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa kati ya pauni milioni 25 hadi 30. (Daily Mail).
Ozan Kabak
KLABU ya Crystal Palace wanajadiliana na Schalke kuhusu mkataba wa mlinzi wa Uturuki, Ozan Kabak (21). Huenda akagharimu kati ya pauni milioni 10-12. (Guardian).
Jesse Lingard
EVERTON imeungana na orodha ya klabu zinazofuatilia hali ya mshambuliaji, Jesse Lingard (28) hapo Manchester United. (Sun).
Ross Barkley
MENEJA wa West Ham, David Moyes atamgeukia kiungo wa Chelsea Muingereza Ross Barkley (27), ikiwa klabu hiyo itashindwa kumsajili Lingard. (90min).
Mario Lemina
KLABU ya Newcastle ina matumaini ya kuafikiana na Southampton kuhusu mkataba wa pauni milioni nne wa kiungo raia wa Gabon, Mario Lemina (27),wiki hii. (Daily Mail).
Donny van de Beek
KIUNGO wa Uholanzi, Donny van de Beek (24), amedhamiria kubakia Manchester United msimu huu wa joto licha ya kutakiwa na klabu za Italia, Hispania na Ujerumani. (Manchester Evening News).
Lewis Bate
LEEDS United wanakaribia kumsajili kiungo wa Chelsea, Muingereza Lewis Bate (18). ‘The Blues’ wanatarajiwa kujumuisha kifungu cha sheria kitakachoongoza kuuzwa kwake lakini sio cha kumnunua tena akiondoka. (Leeds Live).
Manuelli Locatelli
JUVENTUS wanakaribia kufikia makubaliano na Sassuolo kuhusu mchezaji, Manuel Locatelli (23). (Corriere dello Sport).