Gabriel Jesus
MANCHESTER City wapo tayari kumtoa mmoja wa wachezaji nyota akiwemo mshambuliaji wa Brazil, Gabriel Jesus (24), nahodha wa Algeria, Riyad Mahrez (30), kiungo wa Ureno, Bernardo Silva (26), au mshambuliaji wa Uingereza, Raheem Sterling (26), kama sehemu ya mpango wa kuishawishi Tottenham kuwauzia nahodha wa England, Harry Kane. (FourFourTwo).
Harry Kane
MSHAMBULIAJI, Harry Kane atapokea kitita cha pauni 400,000 kwa wiki atakapojiunga na Manchester City baada ya mwenyeiti wa Tottenham, Daniel Levy, kuidhinisha kuondoka kwake wiki iliyopita. (Sun).
Kylian Mbappe
MSHAMBULIAJI wa Ufaransa, Kylian Mbappe (22), hatakubali mkataba mpya Paris St-Germain kwani anajiandaa kuhamia Real Madrid, licha ya klabu hiyo ya Ufaransa kutaka kumuunganisha na mchezaji mwenzake wa kimataifa, Paul Pogba. (Marca).
Raphael Varane
MANCHESTER United pia wanang’ang’ania kufikia makubaliana na Real Madrid kumsajili beki wa Ufaransa, Raphael Varane (28). Klabu hiyo ya La Liga inataka kulipwa pauni milioni 50 kumuachia mlinzi huyo huku United wakiwa tayari kulipa pauni milioni 40. (Mirror).
Franck Kessie
LIVERPOOL ni miongoni mwa klabu kadhaa za Ulaya zinazotafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa AC Milan na Ivory Coast, Franck Kessie (24). (Gazzetta dello Sport).
Mario Lemina
KLABU ya Newcastle ina imani ya kumpata kiungo wa Southampton na Gabon, Mario Lemina (27), baada ya kufanya mazungumzo na wachezaji kadhaa wa kiungo ambao bei yao iko nje ya viwango vya mshahara wa klabu hiyo. (Northern Echo).
Eden Hazard
MSHAMBULIAJI, Eden Hazard (30), tayari ameonesha wazi hisia zake kwamba kurejea kwake Chelsea haina mjadala baada ya vyombo vya habari vya Hispania kuripoti kuwa Real Madrid inatafuta njia ya kumuuza. (Mirror).
Aaron Ramsdale
ARSENAL imeambiwa na Sheffield United kuongeza ofa ya kumnunua, Aaron Ramsdale (32), hadi pauni milioni 32 baada ya kukataa mara mbili dau la kumuuza kipa huyo. (Times).
Sergio Romero
CHELSEA pia wanamtaka kipa Muargentina, Sergio Romero (34), baada ya mkataba wake na Manchester United kukamilika huku ‘The Blues’ wakiendelea kumtafuta mchezaji wa tatu ambaye anaweza kushikilia nafasi ya Edouard Mendy na Kepa Arrizabalaga. (Telegraph).
Granit Xhaka
KIUNGO wa Arsenal, Granit Xhaka anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Roma baada ya klabu hiyo ya ‘Serie A’ kuonesha ishara kwamba inamtaka ajiunge nao katika mechi ya kabla ya msimu huko Ureno wiki ijayo. (Daily Mail).
Julian Alvarez
KLABU ya Aston Villa huenda wakawasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji wa River Plate na timu ya taifa ya Argentina, Julian Alvarez wiki ijayo. (TNT Sports).
Cameron Carter-Vickers
MLINZI wa Tottenham na Marekani, Cameron Carter-Vickers (23), huenda akajiunga na Newcastle, ambao wanamtafuta mchezaji nyuma baada ya Brentford kushinda kinyang’anyiro cha kumsajili mlinzi wa Celtic na Norway, Kristoffer Ajer (23). (90Min).
Domenico Berardi
KLABU ya Leicester City ni miongoni mwa vigogo kadhaa vinavyomtaka mshambuliaji wa Italia, Domenico Berardi anayeichezea Sassuolo mwisho wa msimu ujao (Gazzetta Dello Sport).
Billy Gilmour
KLABU ya Norwich City inakaribia kumsaini kwa mkopo kiungo wa Scotland, Billy Gilmour (20) kutoka Chelsea. (Sky Sports).
Otavio
LIVERPOOL huenda ikamsaini mshambuliaji wa Porto na Brazil, Otavio (26), kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho kutokana na kifungo kinachomzuia cha pauni milioni 34. (Star).
Matthew Cox
KLABU ya Aston Villa na Norwich zinajaribu kumsaini kipa wa England mwenye umri wa miaka 18, Matthew Cox kutoka klabu ya daraja la kwanza AFC Wimbledon. (Football Insider).
Markus Schopp
KLABU ya Barnsley ipo katika mazungumzo na meneja wa TSV Hartberg , Markus Schopp, kuhusu uwezekano wa kocha huyo wa Austria kuwa bosi mpya kutokana na kuondoka kwa Valerien Ismael kutimkia West Bromwich Albion. (Sky Sports).