ERLING BRAUT HAALAND
CHELSEA inatarajiwa kutoa dau la pauni milioni 130 kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 22, baada ya mmiliki wake Roman Abrahamovich kutoa baraka zake kuendelea na kile ambacho kitakuwa rekodi mpya ya klabu hiyo.. (Football Insider)
ROMELU LUKAKU
INTER MILAN inataka dau lisilo chini ya pauni milioni 102.5 kutoka Chelsea ili kumuuza mshambuliaji wa Ubeligiji Romelu Lukaku, 28, iwapo The Blues watashindwa kumsajili Haaland. (Metro)
JACK GREALISH
MANCHESTER CITY wameafikia makubaliano na kiungo Jack Grealish na iko tayari kuipatia ofa ya £90m Aston Villa ili kumsajli mchezaji huyo wa England, 25. (Football Insider)
HARRY KANE
MANCHESTER CITY inasema kwamba ripoti zinazosema kwamba klabu hiyo imeafikiana na Tottenham kumsaini mshambuliaji wa England Harry Kane kwa dau la £160m ni upuzi (Manchester Evening News)
HARRY KANE
TOTTENHAM imesisitiza kwamba haina mpango wa kumuuza nahodha huyo wa timu ya taifa ya England msimu huu. (Football London)
HARRY KANE
MANCHESTER CITY imefanya makubaliano ya kibinafsi na Harry Kane ambaye atakuwa analipwa £350,000 kwa wiki na iko tayari kulipa zaidi ya pauni milioni 120. (Star)
PAUL POGBA
MANCHESTER UNITED inasubiri ombi kutoka kwa PSG msimu huu la kumtaka kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 28. (Telegraph)
KYLIAN MBAPPE
MSHAMBULIAJI wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, ameiambia PSG kwamba hatoongeza mkataba wake ambayo unakamilika 2022, na hivyobasi anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu
EDUARDO CAMAVINGA
KIUNGO wa kati wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga anataka kuhamia Uhispania baada ya mazungumzo kati ya Manchester United na wawakilishi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 kutofua dafu. “. (Manchester Evening News)
CRISTIANO RONALDO
BARCELONA inaamini kwamba iwapo mshambuliaji wa Portugal Cristiano Ronaldo ataondoka Juventus msimu huu, klabu hiyo ya Itali itakuwa tayari kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann kukiwa na sheria ya kumnunua kabisa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Sport – in Spanish)
JOAN LAPORTA
RAIS wa Barca Joan Laporta anasema kwamba klabu hiyo inamthamini sana Antoine lakini kuna soko lake na kwamba mabingwa hao wa Uhispania wako tayari kwa mapendekezo yote. (Goal)
ALEXANDRE LACAZETTE
ARSENAL haitamuongezea kandarasi mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette na imetoa ofa ya dau la £15m kwa mchezaji huyo ili kusaidia timu hiyo kupata fedha za kumnunua mshambuliaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 Tammy Abraham.. (Sun)
STEVE BRUCE
MKUFUNZI wa Newcastle United Steve Bruce amesisitiza kuhusu mpango wa klabu hiyo kumsaini kiungo wa kati wa Arsenal mwenye umri wa miaka 21 Joe Willock lakini inasema kwamba klabu hiyo inasubiri Arsenal na Willock kufanya uamuzi kuhusu hatma yake. (Sky Sports)
STEVEN GERRARD
MKUFUNZI wa klabu ya Rangers na aliyekuwa nahodha ya klabu ya Liverpool Steven Gerrard, 41, amesema kwamba alishangazwa baada ya kuhusishwa na kazi ya kuifunza Everton kabla ya usajili wa Rafael Benitez na kwamba mpango kama huo hauwezekani. “. (ESPN)
MOHAMED SALAH
LIVERPOOL inataka kumzuia mshambuliaji Mohamed Salah, 29, kuweka kandarasi mpya huku kandarasi ya raia huyo wa Misri ikitarajiwa kukamilika 2023. (Liverpool Echo)
HARRY WILSON
FULHAM inakaribia kumsajili winga wa Liverpool na Wales Harry Wilson kwa dau la £10m. (Sun)