Yoshinori Muto
MSHAMBULIAJI wa Newcastle raia wa Japan, Yoshinori Muto (29), yuko kwenye mazungumzo ya kujiunga na Aris Salonika ya Ugiriki baada ya msimu uliopita kucheza kwa mkopo kwenye klabu ya Hispania ya Eibar. (Newcastle Chronicle).
Cristiano Ronaldo
JUVENTUS wamemueleza, Cristiano Ronaldo (36) kwamba wanatarajia asalie klabuni hapo msimu huu. Mshambuliaji huyo Mreno, amekuwa akihusishwa kutaka kutimka wakati huu ambapo mkataba wake ukisalia na mwaka mmoja kuisha. (Sky Sports).
Aaron Ramsey
KLABU ya Juventus imeonyesha nia ya kumuuza, Aaron Ramsey (30) msimu huu, kiungo huyo wa Wales, anaonekana kama mzigo kwa klabu kwa sababu ya mshahara wake mkubwa. (Gazzetta dello Sport).
Raphael Varane
MANCHESTER United watamsajili beki wa Real Madrid na Ufaransa, Raphael Varane kwa mkataba wa miaka minne na uwezekano wa kuongeza mwaka mwengine mmoja, lakini, haifahamiki hasa ni lini beki huyo mwenye umri wa miaka 28 atafanyiwa vipimo vya afya kwa sababu ya masharti ya ‘corona’ ya kukaa ndani. (Athletic).
Axel Tuanzebe
KLABU ya Newcastle inapambana kukamilisha usajili wa beki wa zamani wa timu ya taifa ya vijana ya England chini ya umri wa miaka 21, Axel Tuanzebe (23), kutoka Manchester United. (Telegraph).
Ben White
KIUNGO, Ben White (23) anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Arsenal huku uhamisho wa mlinzi huyo wa England wa pauni milioni 50 ulisharidhiwa na Brighton tangu wiki iliyopita. (Sky Sports).
Romelu Lukaku
MSHAMBULIAJI, Romelu Lukaku (28), anafuraha Inter Milan na nyota huyo wa Ubelgiji, hana mpango wa kuondoka klabuni hapo msimu huu, licha ya Chelsea kuonyesha nia ya kumtaka. (Express).
Cristiano Romero
KLABU ya Tottenham wanaongeza nguvu ya kujaribu kumnasa beki wa Atalanta na Argentina, Cristian Romero (23), kwa ada ya pauni milioni 40. (Telegraph).
Leon Bailey
OFA ya Aston Villa ya kumsajili winga wa Bayer Leverkusen Mjamaica, Leon Bailey, imeanza kuwa ngumu kufuatia klabu za Leicester, Everton, Wolves na Southampton kuonyesha nia ya kumtaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, anayepatikana kwa ada ya pauni milioni 30. (90min).
Antoine Griezmann
BARCELONA hawajapokea mpaka sasa maombi yoyote ya usajili kwa ajili ya mshambuliaji wao Mfaransa Antoine Griezmann (30). (Marca).
Xherdan Shaqiri
KIUNGO, Xherdan Shaqiri (29), anajiandaa kutimka Liverpool msimu huu, huku Napoli na Lazio ni baadhi ya klabu zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili winga huyo wa Switzerland. (Goal).
Matchoi Djalo
ARSENAL wanafikiria kumsajili winga wa Kireno, Matchoi Djalo (18), kutoka Pacos de Ferreira anayepatikana kwa ada ya pauni milioni moja. (Sun).
Jens Styger Larsen
KLABU ya West Ham wameonyesha nia ya kumsajili mlinzi wa Denmark, Jens Styger Larsen (30), ambaye yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Udinese na anaweza kugharimu pauni milioni 4.2. (Football.London).
Marko Arnautovic
MSHAMBULIAJI wa zamani wa West Ham na Stoke, Marko Arnautovic (32), atawasili Italia wiki hii – Muaustria huyo anakamilisha uhamisho wake kutoka Shanghai Port ya China kwenda Bologna. (Corriere dello Sport – in Italian)
Sam Vokes
KLABU ya Wycombe ipo katika mazungumzo mazuri ya kumsajili mshambuliaji wa Wales, Sam Vokes (31), kutoka Stoke ya Championship. (Football Insider).