Anwar El Ghazi
ASTON Villa itamruhusu winga wa Uholanzi, Anwar El Ghazi (26), kuondoka kwa ada ya pauni milioni 15 kama AS Roma itapekeka ofa kufuatia kuonyesha nia ya kumtaka. (Football Insider).
Paul Pogba
KLABU ya Paris St-Germain imeanza mazugumzo ya awali na Paul Pogba kuangalia kama anaweza kujiunga nao kutoka Manchester United msimu huu ama msimu ujao, wakati kiungo huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 28, atakapokuwa mchezaji huru. (Athletic).
Hector Bellerin
ARSENAL wamemuweka beki wa kulia wa Hispania, Hector Bellerin (26), katika mpango wa kubadilishana na mshambuliaji wa Inter Milan, Muargentina Lautaro Martinez (23). (Football Insider).
Leon Bailey
ASTON Villa imetoa pauni milioni 25.5 kwa ajili ya Leon Bailey (23), lakini, Bayer Leverkusen inataka pauni milioni 29.8 kwa ajili ya winga huyo Mjamaica, ambaye anawawindwa pia na klabu za Leicester City na Wolves. (Bild).
Dusan Vlahovic
KLABU ya Tottenham inamuwania, Dusan Vlahovic kutaka Fiorentina ambayo huenda ikahitaji dau la pauni milioni 50 kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 21. (Telegraph).
Erling Braut Haaland
MSHAMBULIAJI wa Norway, Erling Braut Haaland (21), na winga wa Ujerumani, Julian Brandt (25), watasalia Borussia Dortmund msimu huu. (Tuttosport).
Andre Onana
KLABU ya Ajax imethibitisha kwamba vigogo vya Arsenal na Lyon vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mlinda mlango wake raia wa Cameroun, Andre Onana (25) ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa kwa sababu ya dawa za kusisimua misuli. (Voetbal International).
Christos Tzolis
NORWICH City inajiandaa kutoa kitita cha pauni milioni 10 kwa ajili ya kumsajili winga wa PAOK Salonika, Mgiriki Christos Tzolis (19). (Football Insider).
Ilaix Moriba
KLABU ya Barcelona bado hawajakubaliana mkataba mpya na Ilaix Moriba, yoso wa Kihipsania mwenye umri wa miaka 18, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao na tayari klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England zimeonyesha nia ya kumtaka. (Marca).
Manuel Locatelli
JUVENTUS wanakutana tena na maofisa wa Sassuolo wakiwa na matumaini ya kukamilisha mpango wa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Italia, Manuel Locatelli (23), na wanataka pia kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Kaio Jorge (19), kutoka Santos. (Tuttosport).
Angelo Fulgini
KLABU za Crystal Palace, Newcastle na Monaco ni miongoni mwa vigogo vinavyomtaka kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya miaka 21 anayekipiga Angers, Angelo Fulgini (24). (Mail).
Ruben Neves
MPANGO wa Manchester United wa kumsajili kiungo wa Ureno kutoka Wolves, Ruben Neves (24), upo mbali na kukamilika. (Eurosport).
Toby Alderweireld
TOTTENHAM Hotspurs walimuuza mlinzi, Toby Alderweireld kwenda Al-Duhail ya Qatari kwa ada ya pauni milioni tatu ingawa alikuwa na mkataba wa mpaka mwaka 2023 na akiwa na miaka 32 tu. (Sun).
Josh Doig
KLABU ya Leeds United imeambiwa wanapaswa kutoa pauni milioni tano kama wanataka kumsajili mlinzi wa kushoto wa Hibernia raia wa Scotland, Josh Doig (19) msimu huu. (Leeds Live).
Yasser Larouci
LIVERPOOL imepoteza mamilioni ya pauni baada ya mlinzi wa kushoto, Yasser Larouci (20), raia wa Algeria kuondoka bure kwenda Troyes. (Mirror).
Aaron Leya Iseka
MSHAMBULIAJI wa Ubelgiji, Aaron Leya Iseka (23), anajiandaa kujiunga na Barnsley akitokea Toulouse baada ya msimu uliopita kucheza kwa mkopo Metz. (L’Equipe).