KAMPALA, Uganda
SHIRIKISHO la Soka la Uganda (FUFA) limefanikiwa kunasa saini ya aliyewahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredojevic mwenye umri wa miaka 51 baada ya kutimuliwa Zambia na kumpa mkataba wa miaka mitatu.

Uganda ‘The Cranes’ wamerudi tena kwa Micho raia wa Serbia kufuatia rekodi ambayo aliiacha kwenye viunga hivyo vya kuipeleka Uganda Kombe la Mataifa Bingwa Afrika (Afcon), mwaka 2017.

Na itakumbukwa kipindi hicho, Uganda ilikuwa haijawai kushiriki michuano hiyo kabla kwa takribani miaka 39, ingawa kwa sasa kuna maboresho makubwa ya kikosi kwa ujumla.

Uganda ilikuwa bila ya kocha mkuu tangu kufutwa kazi kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Johnathan Mckinstry.(AFP).