ZASPOTI
CHAMA cha Soka Mkoa wa Mjini Magharibi kimetangaza timu ambazo zimepata nafasi ya kuendelea na ligi hiyo na zile zilizoshuka huku nyengine zikiendelea na hatua ya nne bora.
Katibu wa kamati ya mashindano wa chama cha hicho, Ibrahim NMakeresa, alisema, katiba yao inasema kuwa timu tatu ndizo zinazoshuka na moja ya kupanda.

Alizitaja timu zilizoshuka ni Gulioni City, Ujamaa na Miembeni ambazo zitashiriki ligi daraja la pili wilaya ya mjini.
Alisema timu zilizobakia kwenye daraja hilo ni pamoja na Kundemba FC, Umojambuzini, Muungano Rangers na New City.
Nyengine ni pamoja na Bweleo,Kijangwani, Kikwajuni, Raskazone,Mwembeladu na Nyangobo.

Alisema ligi hiyo inaendelea kwa hatua ya nne bora ambapo timu nne zilifanikiwa kutinga hatua hiyo ni New City, Kundemba FC, Muungano Rangers na Umojambuzini.
Alisema ligi hiyo inatarajiwa kumalizika leo ambapo timu zitakabidhiwa zawadi zao na bingwa ambae atapata nafasi ya kupanda daraja la kwanza kanda.