NA HASHIM KASSIM

KATIBU wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya mjini Alawi Haidar Foum amesema  ujenzi wa ofisi za chama hicho, unaendelea vizuri katika eneo la Amani karibu na uwanja wa mkubwa wa mpira.

Akizungumza na gazeti hili katibu huyo alisema ujenzi wa ofisi hizo unaendelea, na unatarajiwa kukamilika kabla ya uongozi uliopo haujamaliza muda wake ili kuhakikisha soka linakua katika wilaya hiyo.

Alawi alibainisha kuwa jengo hilo  litakuwa na ofisi mbalimbali ikiwemo vijana na litakua na holi ambalo lina uwezo wa kuchukua watu 300, hivyo itarahisisha shughuli zao hasa za mikutano.

“Katika harakati za ujenzi wa ofisi zetu za mpira wa miguu wilaya ya mjini zinaenddelea katika eneo la Amani, tumefikia pazuri na unatarajia kukamilika katika kipindi cha uongozi huu ili watakao kuja baada yetu tuwakabidhi ofisi hizi” alisema.