LONDON, England

WAKATI klabu ya Manchester United ikipiga hesabu ya kuinasa saini ya beki wa Real Madrid, Raphael Varane, Chelsea nayo inatajwa kuiwinda saini ya nyota huyo kuwatibulia mipango wapinzani wao.

Man United ipo kwenye hesabu za kumpata beki huyo na inaelezwa kuwa ipo kwenye mazungumzo ili kumpata nyota huyo ambaye ametwaa mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa Real Madrid.

Dau la pauni milioni 42.8 limewekwa mezani kwa ajili ya kumpata nyota huyo, ambaye mkataba wake unakaribia kumeguka msimu huu.

United inaamini kwamba ikakamilisha mpango wa  nyota huyo itaongeza makali hasa kwenye safu ya ulinzi na inatajwa kumpa ofa ya miaka mitano, huku Chelsea nayo ikielezwa kuwa wamewasilisha ofa yao ambayo haijawekwa wazi.