WAPENZI wasomaji wetu wa Zanzibarleo pendwa leo katika safu yetu hii ya maakuli nimewatayarishia mlo mzuri wa

Basi ili kuupika upishi huu ni lazima kuwa na mahitaji haya yafuatayo ikiwa ni pamoja na vitu husika, vipimo na namna ya kupika.

VIPIMO  

Unga wa ngano vikombe 3

Hamira kijiko 1 ½ cha kulia

Maziwa vijiko 2 vya kulia

Siagi  vijiko 2 vya kulia

Sukari vijiko 3 vya kulia

Chumvi ½ kijiko cha chai

Maji ya vuguvugu (warm)

MAFUTA YA KUKAANGIA

Icing sugar na syrup ya chokoleti ya tayari kwa ajili ya kunyunyuzia

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 

  1. Changanya vitu vyote katika bakuli isipokuwa maji. Changanya vizuri.
  2. Polepole tia maji uchanganye kisha ukande upate donge laini lisiloganda mkononi.
  3. Liache donge liumuke kiasi ya ¾ au saa moja.
  4. Sikuma donge kisha katakata round kutumia gilasi ndogo.
  5. Fanya kishimo katika kila duara unalokata kwa kutumia kifuniko cha chupa.
  6. Choma (kaanga) katika mafuta kwenye karai yaliyoshika moto kisha epua uchuje mafuta.
  7. Saga sukari au tumie icing sugar unyunyuzie baadhi ya donuts na baadhi nyunyuzia syrup ya chokoleti ya tayari.
  8. Ukipenda nyunyuzia visukari vya rangi rangi kwa ajili ya watoto.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

KIDOKEZO:  Viduara ulivyokatia kifuniko cha chupa unaweza kuunda duara nyengine au vikaange kama vilivyo.