ANKARA, UTURUKI
UTURUKI imefuta zaidi vizuizi vyake vya COVID-19 kwa wafanyabiashara hasa nyakati za saa za usiku na siku za Jumapili baada ya idadi ya maambukizo ya kila siku kubaki karibu kesi 5,000.
Vizuizi vya kusafiri kwa mwingiliano na mipaka kwa wageni katika mikahawa na karamu za harusi pia zimeondolewa, ilisema wizara ya mambo ya ndani katika taarifa yake.
Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa matamasha na sherehe pia zimeruhusiwa kwa sharti kwamba muziki lazima umalizike saa sita usiku.
Lakini kuvaa mask kwa wananchi bado ni lazima katika nchi hiyo.
Mnamo siku ya Alkhamis, Uturuki ilithibitisha visa vipya 5,288 vya COVID-19, pamoja na wagonjwa wenye dalili 462, na kuongeza idadi ya visa nchini kufikia hadi 5,430,940.
Taarifa ailisema kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na virusi hivyo huko Uturuki iliongezeka kwa watu 42 hadi 49,774, wakati jumla ya waliopona ilipanda hadi watu 5,300,504 baada ya watu wengine 6,219 kupona katika masaa 24 yaliyopita.
Aidha taarifa katika siku iliyopita, imeonesha vipimo waliofanyiwa watu nchini Uturuki vilifikia 61,012,512.
Uturuki ilianza chanjo yake ya COVID-19 mnamo Januari 14 baada ya mamlaka kuidhinisha utumiaji wa dharura wa chanjo ya Sinovac ya Wachina. Zaidi ya watu 35,125,000 wamepewa chanjo hadi sasa.
Uturuki iliripoti kesi yake ya kwanza ya COVID-19 mnamo Machi 11, 2020.