KABUL, AFGHANISTAN

KARIBU raia 2,400 wa Afghanistan wameuawa na kujeruhiwa mnamo Mei na Juni wakati mapigano kati ya vikosi vya usalama vya Taliban na Afghanistan yaliongezeka.

Ujumbe wa UN wa Usaidizi kwa Afghanistan (UNAMA) ulisema katika ripoti ilikuwa imeandika majeruhi ya raia 5,183 kati ya Januari na Juni, ambapo 1,659 walikuwa wamefariki.

Idadi hiyo ilikuwa juu kwa asilimia 47 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana.

Takwimu hizo zilisisitiza hali mbaya kwa raia wa Afghanistan wakati mapigano makali yalipoanza Mei na Juni baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kutangaza wanajeshi wa nchi hiyo watajiondoa ifikapo Septemba, na kumaliza miaka 20 ya uwepo wa jeshi la kigeni nchini humo.

Ninawasihi viongozi wa Taliban na Afghanistan wazingatie njia mbaya na ya kutisha ya mzozo na athari yake mbaya kwa raia, “alisema Deborah Lyons, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan.

Umoja wa Mataifa ulionya kwamba bila kuongezeka kwa vurugu kubwa nchi hiyo iko njiani kurikodi idadi kubwa zaidi ya majeruhi wa raia kwa mwaka mmoja.

Utafiti uliofanywa na shirika la habari la DPA katikati ya Julai ulieleza kwamba Taliban sasa inadhibiti zaidi ya nusu ya wilaya za Afghanistan wakati ikishinikiza kusonga mbele kuelekea miji mikuu kadhaa ya mkoa.