ADDIS ABABA, ETHIOPIA

JIMBO la Ethiopia la Amhara limetoa wito kwa vijana wote kuchukua silaha dhidi ya wapiganaji wa Tigray ambao wanapambana na jeshi la serikali kuu pamoja na wanajeshi wa majimbo mengine tisa.

Wito huo wa hamasa kubwa dhidi ya wapiganaji wa Tigray ambao jeshi la Amhara limesema wanalishambulia sasa , waliendelea na vita vya zamani vya miezi nane na vurugu katika taifa hilo la pembe ya Afrika.

“Ninatoa wito kwa vijana wote, wanamgambo na wasiokuwa wanamgambo, kuchukua silaha yoyote ya serikali, kuchukua silaha zao binafsi, na kujiunga na operesheni ya vita dhidi ya TPLF”.

Vita vilizuka mwezi Novemba kati ya jeshi la Ethiopia na chama cha TPLF ambacho kinaongoza jimbo hilo la kaskazini mwa nchi.

Wiki tatu baadaye, serikali ilitangaza ushindi ilipoteka mji mkuu wa Tigray, Mekelle, lakini TPLF waliendelea kupigana. Mwishoni mwa mwezi Juni, TPLF walidhibiti Mekelle na eneo kubwa la Tigray baada ya wanajeshi wa serikali kuondoka.