NA MWANAJUMA MMANGA

MWENYEKITI  wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Iddi Ali Ame, aliwaomba Wabunge na Wawakilishi wa Viti Maalumu wa Mkoa huo, kuwawezesha wanawake kupitia vikundi vya ushirika ili  waweze kuondokana na utegemezi.

Akifungua kikao cha Baraza la Umoja wa Wanawake Mkoa huo  Ofisi  za CCM  Mahonda, alisema iwapo viongozi hao watawasaidia wanawake  wenzao wataweza kufikia  maendeleo na kukuza uchumi wa nchi kwa kuweka mipango kazi katika vikundi vyao

Aidha, aliutaka uongozi wa umoja wa wanawake kuwahamasisha wanawake wenzao kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi katika chama, ili kuweza kuwatumikia wananchi.

“Ninataka wanwake kuacha tabia ya kujibweteka na badala yake kujituma ili kuleta maendeleo yao ”alisema.

Alisema wanawake wananafasi nzuri ya kuongombea hasa zile za viti maalaum na kuwataka kutoa ushirikiano na viongozi wa jimbo, ili kuona wanaleta maendeleo makubwa katika jumuiya hiyo, sambamba na kusonga mbele.

Walisema watahakikisha katika kuleta maendeleo wataendelea kuongeza namba kwa wanachama wa Chama hicho, ili kuona uchaguzi wa mwaka 2025, wanaimani watashinda kwa asilimia kubwa.