NA ASHA MAULID, IMMZ
ONGEZEKO la Uvamizi wa vibanda vya masoko na Mikahawa maeneo ya Hifadhi ya Taifa Jozani, hivi Karibun umekua ni chanzo cha kupungua watalii wanaongia ndani ya Hifadhi hiyo siku hadi siku.
Hayo yamebainika wakati Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Misitu, Said Juma Ali, akizungumza na watembezaji Wageni ndani ya ukumbi wa Hifadh ya Jozani Ghuba ya Chwaka Mkoa wa Kusni Unguja.
Watembezaji wageni ndani ya Msitu huo, walieleza changamoto mbali mbali ikiwemo ya uvamizi wa eneo hilo, uchafuzi wa barabara na kushuka idadi ya watalii, jambo ambalo linapoteza taaswira ya Uhifadhi wa wanyama pori na Mazingira yao.
Walisema kuongezeka kwa ujenzi wa mabanda kila siku unachangia uchafuzi wa Mazingira ya eneo hilo, kwani kumekuwa na utupaji ovyo wa taka jambo ambalo ni hatarishi kwa afya baadhi ya wanyamapori.
Walisema hilo ni kutokana na kuwepo kwa Kima weusi ambao hufuata chakula vinavyotupwa na kima Punju hula mikaa inayotoka katika majiko ya wafanyabishara hao.
Walisema kuwepo kwa Kima hao katika mazngira ya biashara ni kushusha hadhi ya kiutalii ndani ya Ghuba, watalii nao hutumia fursa hio kuwapiga picha kiunyume na Utaratibu wa Serikali na kupelekea kukosa tija.
Aidha, walieleza, ujenzi wa Nyumba za makaazi, kilimo cha kutumia mbolea ambazo ni sumu ni hatari kwa Kima, Lakini pia ujenzi wa nyumba za kulala Wageni karibu na Hifadhi hupelekea mkanganyiko kwa wageni na kutofikia lengo la Serikali la kukusanya mapato yake kupitia Ghuba hiyo.
Nae Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Jozani, Aziza Yunus Nchimbi, ameleza suala la uwekaji wa Mabango ya Wawekezaji kwenye barabara kuu na maeneo ya jirani, huleta mkanganyiko kwa wageni, jambo ambalo linasababisha kutofikiwa malengo ya ukusanyaji wa mapato.
“Kuna mabango yanayotumia jina la Jozani Forest, Jozani Chwaka Bay Biosphere na Jozani Forest Private Nature Reserve pamoja na picha za Kima Punju, linaikosesha mapato hifadhi na lengo la serikali linashindwa kufikiwa” alisema.