CAPE TOWN, AFRIKA KUSINI
WAFUASI wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma wameandamana wakitaka kiongozi huyo aachiliwe huru.
Wafuasi hao wamezingira barabara, kuharibu na kupora maduka pamoja na kuchoma gari la kusafirisha magari ya kifahari na gari la shirika la Mpango wa Chakula Ulimwenguni baada ya waandamanaji kuchukua mifuko ya unga wa mahindi.
Zuma alianza kutumikia kifungo chake cha miezi 15 jela kwa kukiuka amri ya mahakama mapema wiki hii.
Aidha ombi lake la kutolewa gerezani siku ya Ijumaa lilikataliwa na mahakama ya mkoa na anampango wa kujaribu tena kuiomba mahakama kuu.
Msemaji wa polisi wa mkoa wa Kwa Zulu, Brigedia Jay Naicker amesema watu 28wamekamatwa kwa mashtaka ya vurugu kwa umma, wizi, uharibifu wa mali na ukiukaji wa kanuni za kudhibiti Covid 19.
Zuma alijisakimisha kwa polisi Jumatano usiku wiki iliyopita wakati ambapo wafuasi wake waliokusanyika nje ya nyumba yake wakitishia vurugu ikiwa rais huyo wa zamani atawekwa gerezani.