TRIPOL, LIBYA

WAFANYAKAZI wa kujitolea kutoka shirika binafsi la Sea-Watch wamewaokoa wahamiaji takribani 100 kutoka hatari baharini kupitia operesheni mbili za uokozi.

Usiku wa Alhamis, mabaharia wa meli ya Sea-Watch 3 waliwaokoa zaidi ya watu 30, wakiwemo watoto wachanga watatu na watoto wengi kadhaa, lilisema jana shirika hilo lenye makao yake mjini Berlin.

Asubuhi ya leo Ijumaa, (jana) mabaharia wameokoa zaidi ya watu 60 katika operesheni ya pili. Sea-Watch ilisema kupitia ukurasa wa Twitter, kwamba watu wengi wamejeruhiwa, na baadhi wanauguza majeraha mabaya.

Shirika lingine la misaada la Uhispania la Open Arms pia limeripoti kuwaokoa watu zaidi ya 150 kutoka bahari ya Mediterania siku ya Alhamisi.

Kawaida wahamiaji hufanya safari hatari kutokea Libya au Tunisia kuptia bahari ya Mediterania wakielekea Ulaya, mara nyingi wakifikia nchini Malta, au Italia, wakitumia mashua zilizochakaa, wakitumai kupatiwa hadhi ya ukimbizi.