NA TATU MAKAME

WAJASRIAMALI wa Zanzibar wametakiwa kujiunga na mfuko wa uchangiaji wa hiari wa ZSSF ili kunufaika na mfuko huo wakati wa uzeeni.

Mkuu wa mfuko wa uchangiaji wa hiari kutoa ZSSF Rajab Haji Machano, alitao wito huo kwenye maonyesho ya wajasriamali yanayoendelea huko Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Mkoa wa Mjini Magharibi.

Alisema mwanachama atakaejiunga na mfuko huo atanufaika iwapo atapata janga au ulemavu pamoja na kupatiwa hifadhi ya jamii utuuzimani.

Alisema mwanachama atapata faida baada ya kuweka fedha kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kujiunga kwenye mfuko, ili ziweze kumsaidia katika mambo madogo madogo ikiwemo ujasriamali.

Hata hivyo, alisema mwanachama atakuwa na uwezo wa kumfungulia mwanafunzi anaeendelea na masomo kuwekewa fedha kidogokidogo hadi atakapofikia umri wa miaka 18 kwa ajili ya kumsaidia kujiunga na chuo.

“Ikiwa mwanafunzi hakupata kuendelea atapatiwa fedha hizo ili zimsaidia kuanzia maisha “, alisema.

Alieleza kuwa mbali na faida hizo pia unaweza kumchangia mtu wako wa karibu kama baba au mama, ili na yeye anufaike.

Akizungumzia kuhusu kima atakachopatiwa mwanachama alisema kulingana na fedha alizoweka akiba tangu atakapojiunga.

“Ikiwa mwanachama ataweka milioni mbili tutampatia shilingi 500,000 na atapata kufanyia huduma zake”, alisema.