NA FATUMA KITIMA, DAR ES SALAAM
OFISA Biashara Mwandamizi  wa TANTRADE, Norah Mishiri , amewaomba wajasiliamali kuhudhuria mikutano ya ana kwa ana yani B2B, ili kuweza kuwapatia uzoefu kwa kubadilishana uzoefu kwenye tasnia hiyo na kuendesha biashara zao.

Rai hiyo ilitolewa kwenye maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa Julius Nyeye maarufu (sabasaba) jijini Dar es Salaam alisema mikutano hiyo ya ana Kwa ana inashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Wafanyabiashara wa  ndani na kutoka  nje .

Alisema pamoja na mambo mengine wadau kwenye sekta ya ngozi wanajitahidi kutengeneza bidhaa hizo ambapo  changamoto kubwa ni Kwa watumiaji.

“Ifike mahala sasa Wananchi hususani watanzania kuunga jitihada ambazo zinafanya na wadau kununua bidhaa za nani zaidi,  ili kuwawezesha  waendelee kuzalisha bidhaa hizo kama vile Viatu shuleni Kwa watoto. mabegi na vitu vinginevyo”alisema