KIGALI, RWANDA

KITUO cha Biomedical Rwanda (RBC) kimewahimiza wajawazito na akina mama wanaonyonyesha kwenda kupata chanjo ya Covid-19.”Tunahimiza wanawake wajawazito na watoa huduma za afya kutokosa chanjo,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa RBC,Dk Sabin Nsabimana alisema kulingana na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), wajawazito wenye dalili wana uwezekano mkubwa wa kuugua ugonjwa mkali, kulazwa hospitali na kufa wakati hawajapewa chanjo.

CDC ilisema kwamba utafiti unaonyesha kuwa watu ambao wamepokea chanjo za Covid-19 wakati wa ujauzito, haswa wakati wa miezi mitatu ya mwanzo, walipitisha kingamwili kwa watoto wao, ambayo inaweza kusaidia kuwalinda baada ya kuzaliwa.

“Wanawake wajawazito hawajaripoti athari baada ya chanjo za mRNA,” Dk. Nsabimana alisema.

Alisema kwamba chanjo za Covid-19 hazijatengenezwa kutoka virusi halisi kwa njia ambayo inaweza kusababisha ugonjwa wowote.”Chanjo haiingiliani na mishipa ya damu ambayo mama hushiriki na mtoto”, alisema.