NAIROBI, KENYA
MAKUNDI ya waandamanaji wenye hasira kali wamepambana na vikosi vya polisi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi wakitaka serikali ya nchi hiyo kuondosha amri ya kutotoka nje.
Pia wameshindikiza kusitishwa kwa baadhi ya masharti yaliyowekwa na serikali, kwalengo la kupambana kuenea kwa virusi vya Corona.
Aidha waandamanaji hao walitaka kumalizika kwa ukatili wa polisi dhidi ya vijana wa taifa wa taifa hilo la Afrika Mashariki.
Inaelezwa kuwa polisi wa nchi hiyo waliwatawanya waandamanaji hao kwa kufyatua risasi hewani, mabomu ya machozi na kuwakamata watu kadhaa.
“Tuko hapa kupinga juu ya vijana wetu jinsi walivyouawa, jinsi wanavyoteseka, Tunataka haki zetu, Vijana wetu hawana kazi, vijana wetu wanauawa, Vijana wetu wanateseka, wameugua kwa sababu ya ukosefu wa kazi, tunamuomba Rais wetu awasaidie vijana wetu.” Alisema Jane Atieno ambaye ni miongoni mwa waandamanaji.
Aidha Serikali ya Kenya kwa sasa imeweka amri ya kutotoka nje nchini kote kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi Alfajiri, hadi Julai 27 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya masharti ya kupambana na COVID-19.
Pia Usafiri wa ndani kwenda maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo umepigwa marufuku, huku mikusanyiko ya umma nayo ikipigwa marufuku kwa sasa.