NA MWANAJUMA MMANGA

WALIMU wa Skuli ya Mpendae, wametakiwa kuongeza juhudi na kuifikisha ipasavyo elimu inayostahiki kwa wanafunzi ili kuwajengea uwezo wa ufahamu na kukabiliana na maisha yao katika jamii.

Aliyasema hayo Ofisa Sekondari, Haroub Ali Hamad, wakati akizungumza katika hafla ya kumuaga mwalimu mstaafu Abdallah Sheria huko Tomondo, ambapo alisema kuwa juhudi za kuwapatia elimu bora wanafunzi ndio itakayopelekea kuongeza ufaulu na kuondokana na uelewa mdogo kwa wanafunzi hao.

Alisema iwapo wanafunzi watapata elimu wataweza kuwasaidia wenzao na kuongeza kiwango cha ufaulu katika skuli zao pia kuweza  kufikia malengo waliyojiwekea hapo baadae.

Hivyo aliwataka walimu waliobakia kufanya kazi kwa kujititolea kwani ndio njia pekee ya kuweza kumnyanyua mwanafuzi kupafanya vizuri masomo yao.

“Mwalimu akiwa darasani anatakiwa kufundisha kama vile alivyopatiwa mafunzo kwa vitendo, ili kuweza mawanafunzi kufahamu vizuri” alisema Mwalimu huyo.