MADRID, UHISPANIA

IBADA ya kumbukumbu ya wahanga wa vifo vya corona imefanyika katika Ikulu ya Royal hapo juzi nchini Hispamia.

Ibada hiyo maalumu ni ya kuwakumbuka watu 81,043 ambao wamepoteza maisha yao kwa ugonjwa wa corona.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na Mfalme Felipe VI na Malkia Letizia wa Uhispania, Waziri Mkuu Pedro Sanchez na viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa.

Wanafamilia wa wafanyikazi wa afya 102 waliopoteza maisha kutokana na corona  huko Uhispania pia, sambamba na kumbukumbu hiyo lakini pia kulikuwa na hafla ya kutoa medali kwa jamaa wa wahudumu wa afya waliopoteza wapendwa wao kwa ugonjwa wa corona.

Anceli Hidalgo mwenye umri wa miaka 97, ambaye alikuwa mtu wa kwanza kupewa chanjo dhidi ya COVID-19 huko Uhispania mnamo Desemba 27, 2020, alitoa ujumbe katika hafla hiyo. Alishukuru wafanyakazi wa afya, wahudumu wa nyumbani na madereva wa gari la wagonjwa, akisema “kazi na juhudi zao zinaokoa maisha mengi.” Aliwataka pia vijana ambao hawajachanjwa “waheshimu janga hilo.”

Mfalme Felipe VI alitoa heshima katika hotuba yake kwa wafanyikazi wa afya ambao “walitoa huduma bora kwa wagonjwa’.

“Tunapaswa kukumbuka wale wote ambao hawapo nasi tena na tunaonyesha   heshima yetu kwa wafanyikazi wa afya, ambao wametoa kila kitu tangu mwanzo wa janga hilo.”

“Hakuna maneno ambayo yanaweza kutoa faraja kwa kweli kwa kumpoteza mpendwa, lakini una heshima yetu ya kuwakumbuka wapendwa wetu kwa hisia kali,” alisema, huku akionya janga hilo bado halijafika mwisho.

Katika hafla hiyo, Maria Diaz, mfanyakazi wa afya, alielezea matumaini ya siku zijazo katika nchi ambayo asilimia 47.4 ya idadi ya watu wamepokea dozi zote mbili za chanjo na asilimia 60 wakiwa wamechanjwa mara moja.

“Chanjo imeturuhusu kufikiria juu ya maisha bora ya baadaye. Sayansi imeshinda mara nyingine tena,” alibainisha.

Takwimu za hivi karibuni kutoka kwa Wizara ya Afya zilithibitisha visa vipya 26,390 vya COVID-19 katika kipindi cha masaa 24 hadi juzi, na kiwango cha matukio ya siku 14 kimeongezeka hadi kesi 469.50 kwa kila wakazi 100,000, na kiwango cha matukio katika 1,508.64 kwa kila 100,000 kwa wale wenye umri wa miaka 20-29.