KIGALI, RWANDA
WANAFUNZI wa shule za msingi nchini Rwanda wameanza mitihani ya taifa siku ya Jumatatu wakati taifa hilo likikabiliana na wimbi baya la mripuko wa maradhi ambukizi ya corona nchini humo.
Wizara ya elimu imesema wanafunzi waliopata maambukizi ya virusi vya corona watafanya mitihani yao katika vyumba tofauti na wenziwao.
“Kwa bahati ni kuwa hakuna mwanafunzi ambaye yuko mahututi,” alisema waziri wa elimu Valentine Uwamariya wakati akizungumza na chombo cha habari cha taifa hilo.
Inaelezwa kuwa wanafunzi wanafanya mitihani katika vituo 1,021 kwa taifa zima, ni zaidi ya wanafunzi 100 kwa miaka miwili iliyopita, ikiwa lengo kuu ni kuruhusu watu wakae mbalimbali.
Aidha wizara hiyo imeagiza kuwa wanafunzi wenye virusi vya corona wanapaswa kusindikizwa na wazazi au mlezi kwenda kwenye kituo cha mtihani na kumrudisha nyumbani pale watakapomaliza.
Maofisa wa afya nchini Rwanda wamethibitisha wiki iliyopita kuwa uwepo wa dalili za wimbi la Delta , wakati taifa likiwa na wastani wa wagonjwa 800 kwa kila siku katika wiki nne zilizopita.
“Kuna wagonjwa mahututi zaidi na vifo vingi zaidi na hatujawahi kufikia hapa kabla.” Alisema waziri wa afya wiki iliyopita.