NA TATU MAKAME

WANANCHI wa Zanzibar wametakiwa kuacha tabia ya kutupa takataka baharini na badala yake watumie madoo ya taka yanayowekwa kandokando ya bahari, ili kuepusha uharibifu wa mazingira ya bahari na kuleta athari za utalii.

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Zanzibar, Dk. Salum Sudi Hemed, alisema hayo huko Fungu la Pange mara baada ya kumalizika zoezi la usafi lililoandaliwa na watendaji wa Idara ya Maendeleo ya uvuvi na watembeza watalii kwenye fungu hilo.

Alisema utupaji wa takataka katika maeneo hayo yanaharibu mandhari ya fungu hasa ukizingatia kuwa eneo hilo linatumika kwa shughuli za utalii.

“Eneo hilo ni maarufu kwa sasa watalii wanakwenda kufanya utalii na kupata upepo wa bahari kama yalivyo maeneo mengine ya utalii, hivyo tunawataka wananchi na wavuvi waache tabia ya kutupa taka ili kuendeleza usafi maeneo hayo.