ANTANANARIVO, MADAGASCAR

RAIA kadhaa wa mataifa ya kigeni pamoja na wengine wa nchini Madagascar wanashikiliwa na mamlaka kwa tuhuma za jaribio la mauaji ya Rais Andry Rajoelina.

Mwanasheria mkuu wa serikali nchini humo amesema kwenye taarifa yake kwamba raia wawili wa Ufaransa ni miongoni mwa waliokamatwa kwenye taifa hilo la kisiwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi unaohusiana na kudhoofisha hali ya usalama wa taifa pamoja na diplomasia.

Rajoelina alikula kiapo cha urais mwaka 2019 baada ya uchaguzi mgumu ambao ulipingwa kwenye mahakama ya kikatiba kutoka kwa wapinzani wake.