BERLIN, UJERUMANI

WATU wawili wamefariki dunia, 31 kujeruhiwa na wengine kadhaa hawajulikani walipo baada ya kutokea mripuko katika kiwanda cha madawa cha mji wa Leverkusen nchini Ujerumani.

Polisi ya mji huo inasema watano miongoni mwa majeruhi kwa sasa wanapatiwa matibabu.

Meya wa mji huo wa kandoni mwa mto Rhine na wenye viwanda kadhaa vya madawa Mayor Uwe Richrath ameiita Jumanne kuwa ni siku ya maafa kwa wakazi wake.

Wakaazi katika sehemu za karibu na kiwanda hicho walitakiwa kufunga madirisha na milango na wasile vyakula walivyopika  katika maeneo ya wazi au nje ya nyumba zao pamoja na udhibiti wa viwanja vya michezo kwa watoto.

Onyo kama hilo limetolewa hadi mji mwengine wa Dortmund, ulio umbali wa kilometa 60, wataalamu wakionya athari zinaweza pia kutokea.