BEIRUT, LEBANON
WAZIRI Mkuu mteule wa Lebanon Saad Hariri ametangaza kujiuzlu baada ya kushindwa kuunda serikali kwa karibu miezi tisa.
Uamuzi huo umekuja baada ya Hariri kukutana na Rais wa nchi hiyo Michel Aoun, na kusema wameshindwa kufikia makubaliano.
Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Saad Hariri amesema rais Aoun alikuwa ametaka marekebisho yafanyike kwenye safu ya mawaziri aliowapendekeza.
Mwanasiasa huyo amesema wamejadili mambo yanayohusiana na uaminifu, na ni wazi kuwa hakuna chochote kilichobadilika.
Serikali ya Lebanon ilijiuzulu baada ya mlipuko mkubwa ambao ulitokea kwenye bandari ya Beirut mnamo Agosti mwaka jana lakini imeendelea kufanya kazi katika hadhi ya serikali ya mpito.