WASHINGTON, MAREKANI

SHIRIKA la afya duniani limetahadharisha kuwa hali mbaya zaidi ya ugonjwa wa corona itashuhudiwa barani Afrika, huku mataifa mengi ya bara hilo yakikabiliana na aina ya corona inayofahamika kama Covid-19 Delta inayoendelea kusambaa.

WHO imezitaka nchi za Afrika kuzingatia hatua za usalama huku zikijiandaa kwa mpango mpya wa utoaji wa chanjo kwa ajili ya kukabiliana na virusi hivyo.

Pia imeongeza kuwa wiki ya mwisho ya mwezi Juni ilikuwa ni wiki mbaya zaidi kwa maambukizi katika bara la Afrika.

Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Dk. Matsidisho Moeti amesema kuwa maambukizi mapya ya corona yanaongezeka mara dufu kila baada ya siku 18, Ongezeko kubwa la wimbi la tatu la maambukizi linaweza kutokea wiki chache zijazo.

kwa baadhi ya nchi, kama vile Namibia na Tunisia, bado hospitali zinahangaika kukabiliana na idadi kubwa ya wagonjwa.

Inaelezwa kuwa  chini ya asilimia mbili (2%) ya watu wakiwa ndio waliopata chanjo kamili, wengi wataendelea kukabiliwa na hatari ya kuugua corona.

Hata hivyo WHO ina matumaini kwamba misaada kutoka Marekani na nchi nyinginge kupitia mpango wa usambazaji wa chanjo ya Covax utasaidia nchi kuinua kampeni za chanjo.