LONDON,UINGEREZA

SHIRIKA la Afya Duniani, WHO linasema idadi ya vifo vilivyotokana na virusi vya korona kote duniani imeongezeka kwa asilimia 21 ikilinganishwa na wiki iliyopita.

Katika ripoti iliyotayarishwa na WHO, watu 69,000 na zaidi walifariki kote duniani katika wiki ya hadi Julai 25.

Idadi ya kila wiki ya maambukizi mapya iliongezeka kwa asilimia nane na kuzidi milioni 3.8,ikiwa ni ongezeko la wiki hadi wiki kwa wiki tano mfululizo.

Marekani ina idadi kubwa zaidi ya visa vipya kwa wiki vikiwa 500,332, ikifuatiwa na Brazil visa 324,334, Indonesia visa 289,029, Uingereza visa 282,920 na India visa 265,836.

Jumla ya idadi ya watu walioambukizwa kote duniani hadi kufikia Julai 25 ilikuwa zaidi ya milioni 193.

WHO inaonya kuwa ikiwa virusi vitaenea kwa kasi ya sasa, idadi inaweza kuzidi milioni 200 ndani ya wiki mbili zijazo.