NAIROBI, KENYA
CHAMA Chama cha Wiper kimetangaza kuanza maandalizi ya kuondoka kwa muungano wa National Super Alliance (NASA).
Halmashauri kuu ya chama hicho (NEC) ilikubaliana kwa kauli moja kuondoka Nasa.
Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alisema kuwa Wiper sasa iko tayari kuingia katika chama cha OKA, na kukihimiza chama cha ODM kufanya hivyo.
“Tumekubaliana kwa kauli moja kuondoka Nasa na kuunda umoja mkubwa, OKA. Tunaua Nasa lakini sio kuua vyama vyengine kama ODM,tunataka kufanya kazi na ODM, Jubilee na vyama vyengine na tunakaribisha vyama vyengine kwa sababu sisi tutaunda serikali ijayo, “Kalonzo alisema.
Kalonzo pia alisema kuwa ODM hatimaye ilifikia makubaliano na vyama vyengine vya Nasa juu ya njia bora ya kugawana ufadhili wa vyama vya kisiasa.
Aliongeza kuwa vyama vya ushirika vya Kenya Alliance viko wazi kwa vyama vyengine vyenye nia.
Dili la Raila na Kalonzo lingempa Rais Uhuru Kenyatta udhibiti mkali juu ya mipango yake ya kurithi 2022, ambayo imetishiwa na kuibuka tena kwa Ruto na upinzani uliogawanyika.