NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Yanga SC kinatarajia kushuka dimbani Alhamisi kuvaana na Ihefu FC ya Mkoani Mbeya.Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa  Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kabla ya  mchezo  huo na Ihefu walivaana na Simba SC jijini Dar es Salaam  nakuwatandika bao 1-0.Kocha mkuu wa timu hiyo Nasri Nabi alisema wapo tayari kwa mchezo huo  na wamejiimarisha vya kutosha.

Alisema watahakikisha wanamaliza ligi kwenye nafasi nzuri na kujiweka kwenye nafasi ya kushiriki ligi ya Mabingwa wa Afrika msimu ujao.

” Tupo tayari kuvaana na Ihefu mchezo wetu wa Alhamisi ,” alisema Yanga wana  Pointi 70 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bra  wamecheza michezo 32 .