NA TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Haruna Niyonzima anatarajia kuagwa kwa heshima kesho, kwenye mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya timu ya Ihefu .

Mchezo huo wa kumuaga Niyonzima utachezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Haruna Niyonzima raia wa Rwanda na tangu kuanza kukipiga kwenye soka la Tanzania, amecheza timu ya Simba kwa mafanikio na Yanga yenyewe.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana Niyonzima alisema kwamba hajastaafu soka, ila anaagana na Yanga kwa heshima .

Alisema anaagana vizuri na mabosi wake hao kwani anaachana nao na kwa muda ambao ameitumikia klabu hiyo hakuona sababu ya kuondoka kimyakimya.

“Bado nipo kwenye soka na nitaweka wazi muelelekeo wangu hivi karibuni, lakini kwa sasa nawashukuru tu mashabiki na kila mtu kwa ushirikiano ambao nimeonyeshwa ,” alisema