BLOEMFONTEIN, AFRIKA KUSINI
WANASAYANSI nchini Afrika Kusini wanafuatilia aina mpya ya kirusi cha corona ambacho polepole kinazidi kusambaa katika miezi ya hivi karibuni.
Aina hiyo, inayojulikana kama C.1.2., iliripotiwa wiki iliyopita na Kituo cha Utafiti cha KwaZulu-Natal.
Ingawa maambukizi mengi Afrika Kusini yanatokana na kirusi cha aina ya Delta chenye chimbuko lake nchini India, lakini wanasayansi wameanza kutiwa wasiwasi na aina hiyo ya C.1.2 kutokana na kwamba kasi yake ya mabadiliko ni mara mbili ya aina nyengine za virusi ulimwenguni.
Hata hivyo wanasema kasi yake ya maambukizi bado ni ndogo.
Afrika Kusini ni nchi iliyoathirika zaidi na virusi vya corona barani Afrika.
Tangu janga hilo kuanza ulimwenguni, Afrika Kuisni imeripoti maambukizi ya watu milioni 2.7.