NA KHAMISUU ABDALLAH

ALI Juma Ali (20) mkaazi wa Mbuzini, amehukumiwa kutumikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka miwili, pamoja na kulipa fidia ya shilingi 300,000 akishindwa atumikie Chuo cha Mafunzo kwa muda wa mwaka mmoja.

Adhabu hiyo imetolewa na mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe na Hakimu Omar Said, wakati alipokuwa akisoma hukumu ya mshitakiwa huyo, dhidi ya kesi ya shambulio la kuumiza mwili ambalo lilimtia hatiani baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Mshitakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na kesi ya shambulio la kuumiza mwili, kinyume na kifungu cha 230 cha sheria namba 6 ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar.

Kijana huyo alidaiwa kumshambulia Abass Shaaban Shamte kwa kumchinja na kisu katika sehemu za magoti yake ya miguu yote miwili na kumsababishia maumivu makali, kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Tukio hilo alidaiwa kulitenda Novemba 4 mwaka 2019 majira ya saa 1:45 usiku, huko Mbuzini wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

@@@@@