LONDON, England
KLABU ya Arsenal imemsajili kiungo, Martin Odegaard, kutoka Real Madrid kwa ada ya pauni milioni 30 wakati kipa Aaron Ramsdale amemaliza kupima afya kabla ya kuhamia Sheffield United.

Mchezaji wa kimataifa wa Norway, Odegaard (22), alitumia nusu ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo kwenye uwanja wa Emirates.Alicheza mechi 20 kwenye mashindano yote na alifunga magoli mawili.

Mkataba wa mchezaji wa kimataifa wa England chini ya umri wa miaka 21, Ramsdale una thamani ya pauni milioni 24 pamoja na pauni milioni sita zaidi katika nyongeza.
Ramsdale (23), ambaye alicheza mechi 38 za Ligi Kuu England akiwa na ‘Blades’ msimu uliopita, ataungana na Bernd Leno na Runar Alex Runarsson kama makipa wa Arsenal.

“Bado kuna kazi inaendelea, lakini, vipimo vya afya vimekamilika, bado kuna mambo kadhaa ya kusawazisha na Sheffield”, bosi wa Arsenal, Mikel Arteta, alisema.
“Aaron ni kipa mwenye kipaji na uzoefu mkubwa na ana uzoefu wa kimataifa kwa England. Ataleta ushindani na ndiyo tunaotaka kuunda, ushindani wenye afya, ushindani wa ubora katika kila nafasi. Tulimtambua Aaron kama chaguo bora”.(BBC Sports).