LONDON, England
MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema walistahili ushindi katika mchezo wa juzi, ila walishindwa kutumia vyema nafasi walizopata.
Arsenal ikiwa Uwanja wa Emirates ilikubali kunyooshwa kwa mabao 2-0 kuyeyushe pointi tatu.
Huo ni mchezo wa pili kwa Arsenal kupoteza kwa kuwa ule wa ufunguzi walipoteza mbele ya Brentford wakiwa ugenini.
Arteta amesema:”Ilikuwa ni lazima tushinde ila namna hali ilivyokuwa mambo yalibadilika. Kipindi cha kwanza tulikuwa na nafasi ya kushinda ila haikuwa hivyo.
“Walipopata bao wapinzani wetu walizidi kulazimisha kupata ushindi na waliweza kufanya kwa nguvu dakika zote 90, hivyo hamna namna ni mbaya kwetu na ukikumbuka kwamba tuliwakosa wachezaji wetu 8 ama 9 hivi,”.