LONDON, England
KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema, ipo katika kipindi kigumu ambacho hakijawahi kutokea hapo kabla’, baada ya kuweka rekodi ya kuanza vibaya zaidi msimu huu.
Baada ya kufungwa 2-0 na Brentford na Chelsea, Arsenal imepoteza michezo yao miwili ya kwanza ya ligi bila ya kufunga kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Kikosi hicho kimekumbana na ugonjwa wa ‘corona’ na majeraha katika kipindi cha wiki mbili za ufunguzi.”Sidhani kama katika historia ya klabu imewahi kukumbana na kitu kama hichi”, alisema, Arteta.

“Lazima tukabiliane na changamoto hii. Ligi au msimamo hauamuliwi mwezi Agosti. Jambo baya zaidi unaloweza kufanya ni kukata tamaa. Hakika hatutafanya hivyo”.
Arsenal ilipo ni kati ya wakushukishwa daraja, ukiondoa siku ya ufunguzi wa msimu ikiwa ni mara ya kwanza tangu Agosti 1992.”

Lazima ieleweke hali tuliyonayo. Tunawakosa wachezaji tisa, na ni vigumu. Sio wachezaji tisa tu kuna baadhi ya wachezaji wakubwa pia”.Washika bunduki hao walikuwa bila ya nyota wao wawili katika safu ya ushambuliaji, Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette pamoja na Willian na mlinda mlango, Alex Runarsson kwa sababu ya ugonjwa wa ‘corona’ wakicheza dhidi ya Brent.

Aubameyang alikuwa amerudi benchi wakati wa mechi dhidi ya Chelsea, lakini, beki wa kati wa pauni milioni 50, Ben White alikuwa nje baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona.