MADRID, Hispania
KLABU ya Atletico Madrid imethibitisha usajili wa Matheus Cunha kutoka Hertha Berlin ikiwa ‘Los Colchoneros’ walikuwa wakitafuta mshambuliaji.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anaweza kuwa hayuko kwenye sura ya Luis Suarez, badala yake alikuwa na mtindo wa kucheza sawa na ule wa Angel Correa, lakini, ameletwa Atletico kukamilisha lengo la Diego Simeone.

Kuwasili kwake kunakuja baada ya Atletico kushindwa kufikia makubaliano na Fiorentina kwa Dusan Vlahovic, ambaye ni nambari 9 ya kawaida.Mapema katika msimu wa joto, Los Colchoneros pia walikuwa wamejaribu kuona kama wangeliweza kumnasa Antoine Griezmann, ​​lakini, hakuna makubaliano yaliyofikiwa.Cunha aliondoka Brazil akiwa na umri wa miaka 18 alipojiunga na Sion ya Uswisi, lakini, hakukaa hapo kwa muda mrefu kwani kiwango chake kiliwavutia RB Leipzig ambayo ililipa euro milioni 15 kumpata.

Baada ya msimu moja na nusu huko Leipzig, Cunha alihama kwenda Hertha kwa ada ya euro milioni 18. Sasa, miezi 18 baadaye, amekamilisha kuhamia Atletico Madrid. (Goal).KLABU ya Bayern Munich imeibuka na ushindi wa mabao 12 Bremer SV katika mchezo wa raundi ya kwanza ndani ya German Cup.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Weserstadion, shujaa alikuwa ni Eric Maxim Choupo-Moting ambaye alitupia mabao manne dk 8,28,35 na 82. Mengine walifunga Jamal Musiala dk 16 na 48, Jan -Luca Warm alijifunga dk 27, Mali Tillman dk 47, Leroy Sane dk 65,Michael Cuisance dk 80, Bound Sarr dk 86 na Corentin Tolisso dk 88.