NA  TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

KOCHA mkuu wa kikosi cha Azam FC, George Lwandamina ametoa ufafanuzi baada ya kupoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Red Arrows.

Mchezo huo ulichezwa juzi nchini Zambia na Azam walipoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya wababe hao.

Huyo ni mchezo wa pili wa kirafiki kwa timu hiyo tangu kutua nchini  Zambia.

Taarifa ya kocha huyo kupitia vyombo vya habari nchini Zambia alisema lengo lake halikuwa wachezaji kucheza kwa kutumia nguvu kuufanya mchezo wa ushindani.

Alisema alihitaji kuwaona wachezaji wake wanacheza vyema kwa maelekezo maalum, hivyo kila mchezaji alipata nafasi ya kucheza kwenye mchezo huo.

“Bado tupo kwenye maandalizi na hii ni mechi yetu ya pili hatujaanza hata mazoezi ya mpira wenyewe bado tupo kwenye utimamu wa mwili wachezaji wangu bado walikuwa na uchovu,” alisema Lwandamina

Alisema walikuwa wanafanya mazoezi kwa ajili ya utimamu baada hakuhitaji wachezaji wacheze kwa dakika 90